Friday, October 28, 2016
INVITATION MESSAGE FOR PEOPLE TO JOIN SHULETIME
INVITATION MESSAGE FOR PEOPLE TO JOIN SHULETIME
Hi!
Mambo vipi?
Kuna hii website nimeona ni vyema nikushirikishe nikiamini inaweza kuwa yenye msaada kwa namna moja ama nyingine,
Inaitwa Shuletime(http://www.shuletime.com).
kwa ufupi, Shuletime ni tovuti (website) inayolenga kuwaleta pamoja wanafunzi walio katika
hatua (level) mbalimbali za kielimu, yaani shule, vyuo na vyuo vikuu na hata vijana walio tayari katika ajira hapa nchini na kwingineko duniani,
kwa lengo la kuzungumza mambo yote yanayowahusu wanafunzi, elimu, jamii na maisha yetu kwa ujumla.
Nina mifano michache ya jinsi ambavyo Shuletime inaweza kuwa na msaada kwako,
Kupitia forums wanafunzi wanashiriki moja kwa moja katika mazungumzo ambapo wana uhuru wa kuuliza maswali kuhusu mambo wanayohitaji kuyafahamu, kwa mfano mwanafunzi aliye hitimu kidato cha nne ama cha sita anaweza kutaka kujua mambo mbalimbali kuhusu vyuo,shule,masomo na kozi anazotaka kuchagua, hii itawasaidia vijana wengi walio mbali na vyanzo ama watu wanaoweza kuwapa ushauri/taarifa hizi hali ambayo hupelekea kufanya uamuzi usio sahihi sana.
Pia mwanachuo anayejiandaa kutafuta kazi ama kuingia kazini baada ya kuhitimu masomo yake angependa kufahamishwa mambo mengi kuhusu hali halisi ilivyo, namna ya kijiandaa kukabiliana na hali halisi katika soko la ajira ama jinsi ya kujiandaa na mazingira ya kazi.
Kupitia forums za Shuletime tunaamini atapata majibu ya maswali haya na mengine na hivyo kufanya maamuzi sahihi yatakayo badili mwelekeo wa maisha yake na watu wanaomtegemea na mwisho kufanikisha ndoto yake.
Hii ni mifano michache tu ya jinsi Shuletime inaweza kuwa na msaada kwetu sisi wanafunzi kama tukiamua kuitumia kwa lengo lililokusudiwa, unaweza kusoma zaidi hapa ( http://www.bit.ly/HowUsefulShuletimeIs ) jinsi Shuletime inavyoweza kuwa na msaada katika maisha yetu kama wanafunzi na kubadilisha maisha yetu kabisa.
Baadhi ya forums zinazohusu elimu ni kama, MIKOPO YA WANAFUNZI, MITIHANI, SHULE & VYUO, MASOMO & KOZI.
Mbali na elimu, kuna mambo mengine mengi yanayozungumziwa katika tovuti ambayo yanamhusu mwanafunzi moja kwa moja kama vile, mahusiano, afya, teknolojia, burudani, michezo n.k
Unaweza kusaidia kufanikisha lengo la shuletime.com kwa kufanya yafuatayo.
1.Kutembelea http://www.shuletime.com na kujiunga bure kabisa ukitumia dakika chache tu.
2.Kushiriki katika mazungumzo (online discussions) kwa kuandika, kuuliza, kujibu hoja (topics) katika forums za shuletime.
3.Kuwashirikisha na kuwaalika marafiki wengi kadri uwezavyo, kama nilivyokushirikisha wewe, waweza fanya hivyo kupitia emails, groups ama kurasa za facebook na whatsapp ama blogs na njia nyingine zinazoendana na hizi.
4.Kwa kuwa shuletime ni ya wanafunzi kwa ajili ya wanafunzi, unakaribishwa kushiriki kuamua ni namna gani ungependa kuona Shuletime ikiendeshwa hapa http://shuletime.com/memberlist.php?mode=contactadmin
- Share on Facebook
- Share on Twitter
- Share on Google+
by
Click this ===> RAY
Ask any Question about C Programming Language and we shall help you! If you have any question or program you need to be written for your just send me question through my
email: raymkindo02@gmail.com
Available link for download